VISIWA VYA CARRIBEAN VYAHARIBIWA VIBAYA NA KIMBUNGA IRMA


Kimbunga kijulikanacho kama Irma kimeharibifu eneo kubwa katika visiwa vya Caribbean ambapo inakadiriwa watu wapatao saba wamepoteza maisha kutokana na kimbunga hicho huku kukiwa na jitihada mbalimbali za uokoaji licha ya changamoto zinazotokana na kuwepo ugumu wa kuyafikia maeneo mengine.
Kimbunga hicho cha kiwango cha tano ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kwa sasa kinapita kaskazini mwa nchi ya Puerto Rico na zaidi ya nusu ya wakazi wapatao milioni tatu wa nchi hiyo hawana umeme kwa sasa baaada ya kimbunga kusababisha mvua kubwa na upepo mkali.
Kwa mujibu wa maafisa wa Puerto Rico wanasema huenda umeme ukakosekana kwa siku kadhaa vilevile kimbunga hicho chenye nguvu nyingi na upepo wa kasi ya kilomita 295 kwa saa kinatarajiwa kupita karibu na pwani cha Jamhuri wa Dominica leo hii.

(sehemu  ya majengo yaliyozungukwa na maji baada ya mvua kubwa iliyosababishwa na kimbunga irma . Picha kwa hisani ya AFP)


Kabla ya uharibifu huu kwenye visiwa vya Carribean kimbunga Irma kilikwisha leta madhara katika maeneo mbalimbali kama vile kisiwa cha Antigua na Barbuda. ambapo mtu mmoja aliripotiwa kupoteza maisha pia kwa mujibu wa waziri mkuu wa visiwa hivyo bwana Gaston Brown amesema kuwa karibu asilimia 95 ya majengo yaliharibiwa.

No comments:

Post a Comment