Mara nyingi panapokuwepo na mvua kubwa huleta athari kwa watu na mali (Picha na mtandao) |
Meneja huyo amesema kuwa mamlaka ya hali ya hewa inatarajia mvua zitaendelea kunyesha katika maeneo ya mikoa ya Magharibi ambayo ni Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Ruvuma, Lindi, Dodoma na Singida ambazo zilianza kunyesha Novemba zinatarajiwa kumalizika Aprili.
Mbuya amesema maeneo mengine katika mikoa ya Tanzania kutakuwa na mvua za kawaida huku mikoa minne ikiwa na mvua kubwa.
Aidha bwana Mbuya amewataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa mara kwa mara ili wapate mwelekeo wa hali ya hewa na tahadhari wanazotakiwa kuchukua.
No comments:
Post a Comment