JE WAJUA MSIMAMO WA MAKAMPUNI YA CHINA KUHUSU IPHONE 7?

   

 Ikiwa ni siku chache tangu kuingia sokoni kwa simu za  iPhone 7 na iPhone 7 plus na kujipatia umaarufu mkubwa duniani hali imekuwa tofauti huko nchini China kwani kampuni kadha nchini humo  zimetoa onyo kali kwa wafanyakazi wake na kuwataka wasinunue simu hizo.

      Kampuni hizo ambazo zimewapiga marufuku wafanyakazi wao zimedai kuwa  marufuku hiyo ni kwa sababu za kizalendo pia kuwafunza wafanyakazi wake kutopenda sana raha na anasa za dunia kwani simu hizi ni za gharama kubwa
Mwonekano wa simu ya kisasa aina ya iPhone 7 (Picha kwa hisani ya mtandao)

Image copyrightSERA HIYO IMETANGAZWA WAKATI SAMBAMBA NA SIKU YA MAADHIMISHO YA MIAKA 85 TANGU WANAJESHI WA JAPAN WALIPOVAMIA MAENEO YA MASHARIKI MWA CHINA MWAKA 1931.
Msemaji wa kampuni ya Nanyang Yongkang Medicine ambayo ni miongoni mwa kampuni iliyozuia wafanyakazi wake kununua simu hii   Bw Liu amesema, lengo la agizo hilo ni kuwahamasisha wafanyakazi kujali zaidi familia zao badala ya kuhangaikia vitu vya anasa.
    Mbali ya kampuni hiyo hospitali ya Fuling Xinjiuzhou Gynecology Hospital  ya mjini Chongqing imewaonya  wafanyakazi wake wasinunue iPhone7. kwani bei yake ni ya juu mno ukilinganisha na simu nyingine.
 Pia ili kuendeleza utamaduni kwa kutopenda matumizi ya anasa na kutumia pesa kwa busara, wasimamizi wa hospitali wamefikia uamuzi wa kuwapiga marufuku wafanyakazi wetu wasinunue simu za iPhone7.
        Kwa upande mwingine baadhi ya watu wamekuwa na mtizamo tofauti na kutoa mtizamo wao kupitia mtandao wa  Weibo  wameeleza kwamba kususia iPhone7 huenda kukawa kunawadhuru Wachina wenyewe kwani uzalishaji wa simu za Apple hufanywa katika viwanda vya kampuni ya Foxconn nchini China.
    Baadhi ya watu wanaotetea uzalendo wa Wachina wamekuwa pia wakipinga simu za iPhone kuonyesha kutoridhishwa kwao na uamuzi wa jopo la kimataifa uliosema China haina haki ya kumiliki visiwa ambavyo imekuwa ikidai katika bahari ya South China Sea hivyo kusababisha baadhi yao kuharibu simu zao hadharani kama sehemu ya kupinga hilo
iphone
Baadhi ya watu wanaounga mkono uzalendo wa nchi ya china wakiharibu simu zao hadharani kama sehemu ya kuunga mko uzalendo. (Picha kwa hisani ya mtandao wa WEIBO)

Huo ndio uzalendo wa wananchi wa china kuhusu bidhaa za Apple hususani simu mpya za iPhone 7 na iPhone 7 plus je unadhani wanachofanya kitaathiri vipi biashara na uchumi kwa ujumla

No comments:

Post a Comment