WABUNGE WAJIUZURU KISA KASHFA YA RUSHWA

Ikiwa ni miezi kadhaa kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini korea kusini hali imeanza kuwa tete hii ni baada ya wabunge ishirini na tisa  wa chama tawala kujiondoa katika chama.
Wabunge hao wamefikia hatua hiyo kufuatia tuhuma za rushwa zinazomkabili rais wa nchi hiyo Park Geun-hye ambaye mbali na rushwa pia anakabiliwa na tuhuma ya  kutumia madaraka vibaya.
  Huenda wabunge hao wakaunda  chama kingine kipya na upo uwezekano wa kumtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayemaliza muda wake Ban Ki-Moon, kuwa mgombea wa chama hicho.
Bwana BAN KI MOON amemaliza muhula wake wa pili akiwa kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  mwishoni mwa mwezi novemba mwaka huu na ameonesha nia ya kurudi nchini korea ili akawatumikie raia wa nchini mwake
Ikiwa hali ndio hii unadhani nini hatma ya korea? 

No comments:

Post a Comment