KANISA LA WASABATO LAFANYA MABADILIKO YA MAENEO YA KAZI KWA BAADHI YA WACHUNGAJI WAKE


(Jengo la makao makuu ya jimbo la mashariki kati mwa Tanzania  ( Picha na Uncle Prince) 



 Kanisa la waadventista wa sabato jimbo la mashariki kati mwa Tanzania  limetangaza mabadiliko ya
 vituo vya kazi kwa baadhi ya  wachungaji wake .  

Akizungumzia mabadiliko hayo mkurugenzi wa Idara ya mawasiliano wa jimbo hilo 
Mchungaji Izungo amesema mabadiliko hayo  yametokana na vikao vya mwisho wa Mwaka vya 
kamati kuu ya Jimbo. 
Wachungaji hao waliobadilishiwa vituo ni
  • Pr.Shauri anayekwenda mtaa wa Kondoa, mkoani Dodoma
  • Pr.Martinus anayekwenda ntaa wa Mlali,
  • Pr.Manyasi anayekwenda mtaa wa Pwaga,
  • Pr.Bunga anayekwenda mtaa wa Mpwapwa,
  • Pr.Shayo anayekwenda kuwa mchungaji sekondari ya kanisa Kitungwa,
  • Pr.Kibasisi anayekwenda mtaa wa Gairo,
  • Pr.Lawi anayekwenda mtaa wa Kilosa,
Mchungaji Andrew Izungo amesema wachungaji wengine ni
  • Pr.Imani anayekwenda mtaa wa Mikese mkoani pamoja na Pr.Shashnale ambaye naye
 anakwenda mtaa wa Ifakara,
  • Pr.Bigambo anayekwenda mtaa wa Kunduchi,
  • Pr.Moses  anayekwenda mtaa wa Bunju,
  • Pr.Charles Mjema  anayekwenda mtaa wa Mwenge,
  • Pr.Stephen Letta aliyekuwa mchungaji wa mtaa wa Mwenge anahamia mtaa wa Tegeta,
  • Pr.David Mmbaga aliyekuwa  mchungaji wa mtaa wa Tegeta anahamia mtaa wa Dodoma,
  • Pr.Bomani anayekwenda mtaa wa Kizota,
  • Pr.Ombeni anayekwenda mtaa wa Kilombero mkoani Morogoro
  • Pr.Methsela anakwenda kuwa mchungaji wa mtaa wa  Mtimbila.
Wengine ni
  • Pr.Saguda anayekwenda kuwa mchungaji wa mtaa wa Malinyi,
  • Emmanuel  Nzota  anayekwenda kuwa mchungaji wa mtaa wa Mlimba
  • Pr.Masunya anayekuwa mchungaji wa mtaa wa Kinondoni,
  • Pr.Kibaso anayekuwa mchungaji wa mtaa wa Jamaica,
  • Pr.Petro Mganda anayekuwa mchungaji wa mtaa wa Morogoro Mjini
Ikumbukwe kuwa kazi ya uchungaji ni wito hivyo basi tunaamini kuwa Mungu ataendelea
 kuwatumia wachungaji hawa katika kazi yake .

No comments:

Post a Comment