Mheshimiwa Joel Bendera Hatunaye tena

 
Mheshimiwa Joel Bendera (Picha kwa hisani ya mtandao)


Hali ya majonzi na simanzi imetawala sehemu mbalimbali za jamhuri ya muungano wa Tanzania kufuatia kifo cha mkuu wa mkoa wa Manyara mstaafu Mh Joel Bendera aliyefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) hapo jana

Akithibisha kutokea kwa kifo hicho  msemaji wa hospitali ya taifa Muhimbili Aminiel Aligaesha ambaye ni msemaji wa hospitali hiyo  amesema, “Ni kweli Joel Bendera amefariki aliletwa leo (jumatano) na gari la wagonjwa saa 6:30 mchana na ilipofika saa 10:24 jioni alifariki.”

Mh Bendera mbali ya ukuu wa mkoa, amewahi  pia kuwa mbunge wa Korogwe Mjini na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo katika utawala uliopita wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.

Mh Bendera alikuwa miongoni mwa wastaafu katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa yaliyofanywa na Rais John Magufuli Oktoba 26,2017 na nafasi yake kuchukuliwa na  Mh Alexander Mnyeti aliyekuwa mkuu wa  Wilaya ya Arumeru.


Mkoani Manyara Mheshimiwa Bendera atakumbukwa kwa moyo wake wa kuhamasisha mazoezi ya viungo na michezo kwa ujumla pia atakumbukwa na wanamichezo wote na wapenzi wa kandada kama kocha bora wa timu ya taifa (TAIFA STARS).

  Pumzika vyema  Mh Joel Bendera 

No comments:

Post a Comment