Parachichi kubwa zaidi duniani lapatikana visiwa vya Hawaii

 
Parachichi tunda adhimu lenye sifa kedekede kiafya na urembo (Picha na mtandao)
Parachichi ni miongoni mwa matunda yanayofahamika na kutumiwa na watu wengi sana hapa Tanzania na kwingineko duniani  mara nyingi  tunda hili hutumika kama kiungo cha mboga,kama  salad pia hutumika kwenye urembo kutokana na faida zake kiafya.

Lakini huko visiwa vya Hawaii nchini Marekani mwanamke mmoja  amepata parachichi kubwa zaidi duniani
Pamela Wang mwanamke kutoka kutoka katika kisiwa cha Big Island anasema akiwa kwenye matembezi aliliona parachichi hilo lenye  kilo 2.35 
Kwa sasa Pamela  Wang amewasilisha ombi rasmi kwa Guinness World Records kutaka  parachichi  hilo litambuliwe kama parachichi kubwa zaidi kuwahi kupatikana duniani.
Mpaka sasa parachichi linaloshikilia rekodi ya dunia kwa ukubwa ni kutoka Venezuela ambalo lina  kilo 2.18 ambalo lilitambuliwa rasmi kuwa kubwa zaidi duniani mwaka 2009
Bi Wang anasema tunda hilo lilitoka kwa mparachichi wa zaidi ya miaka 40 ambao umekuwa karibu na barabara na amesema kuwa lilikuwa tamu sana pia mti wake ni mzuri sana na tunda hilo limeliwa na watu 10 na hawakumaliza hata nusu ya parachichi hilo .
Jimbo la Hawaii, tunda ambalo linatoka kwa tawi lililoning'inia barabarani au linaloanguka barabarani linaweza kuchukuliwa na mtu yeyote yule na liwe lake.
Bi Wang anatarajia kupata majibu kutoka kwa Guinness katika kipindi cha miezi miwili.

No comments:

Post a Comment