Shashi Kapoor aaga dunia kwa ugonjwa wa figo

       

Mwigizaji mkongwe wa India Shashi Kapoor amefariki dunia akitibiwa katika hospitali ya Kokilaben Dhirubhai Ambani mjini Mumbai alipokuwa akipatiwa matibabu ya figo
     Shashi Kapoor atakumbukwa kama mwigizaji maarufu  katika filamu mbalimbali maarufu kutoka India na nje ya india  kama vile Deewar na Kabhie Kabhie, 
        Amekuwa akiugua kwa muda na  siku za karibuni  alikuwa amelazwa hospitali ya Kokilaben Dhirubhai Ambani ya  mjini Mumbai hadi mauti yalipomkuta  akiwa na umri wa miaka 79.

       Mwigizaji huyu  anatoka familia ya Kapoor ambayo imetawala tasnia ya filamu za Kihindi kwa miongo mingi na amefanikiwa kushinda tuzo nyingi za filamu za Bollywood ikiwemo  tuzo ya Padma Bhushan ambayo ni ya heshima aliyopata  mwaka 2011. Kapoor  ameigiza pia katika filamu kadha za Uingereza na Marekani.

     Taarifa ya kifo chake ilipatikana kwa mujibu wa mpwa wake Randhir Kapoor ambaye ameliambia jarida la  Press Trust of India kwamba Kapoor amekuwa akitatizwa na figo kwa miaka mingi.

       Shashi Kapoor alikuwa amemuoa  Jennifer Kendal ambaye ni mwigizaji mwingereza na kwa   pamoja walifanikiwa kuanzisha ukumbi maarufu wa sanaa Mumbai ujulikanao kwa jina la  Prithvi mwaka 1978.

       Shashi Kapoor atakumbukwa kwa filamu zake maarufu kama vile   Haseena Maan Jayegi (1968)  Ek Shriman Ek Shrimati (1969) Kanyadan (1968) Pyar Ka Mausam (1969)  na nyinginezo

No comments:

Post a Comment