Almasi ya Amani yauzwa kwenye mnada jijini Washington

Almasi ni miongoni mwa mawe yenye thamani kubwa ambayo hutumika kwa matumizi mbalimbali(Kwa hisani ya mtandao)
     Almasi ya 14 kwa ukubwa  duniani yenye uzito wa karati 709 ambayo ilipatikana nchini Siera Leone imeuzwa kwenye soko la mnada mjini New York kwa dola milioni 6.5.
      Almasi hiyo imenunuliwa na Laurence Graff ambaye ni mwenyekiti wa Graff Diamonds
Almasi hiyo ambayo imepewa jina la  "peace diamond"  imeuzwa siku ya Jumatatu kwenye mnada 
Ikumbukwe kuwa serikali ya Sierra Leone  ilikataa bei ya dola milioni 7.8 kwenye mnada wa awali mjini Freetown baada ya kusema kuwa bei hiyo ilikuwa ya chini mno ila  sasa inatarajia kutumia pesa hizo kuboresha hali ya maisha katika kijiji cha Koryardu ikiwemo miradi ya maji, umeme, barabara na huduma za afya.
Almasi hiyo ilikabidhiwa kwa serikali ya Sierra Leone mwezi Machi   na Emmanuel Momoh ambaye ni mhubiri wa kikristo.
  Je nini maoni yako katika suala hili?

No comments:

Post a Comment