SHC WAJITOLEA KUJENGA SHULE ILIYOUNGUA MKOANI MBEYA

    Suala la kujitolea kwa ajili ya jamii limekuwa ni jambo ambalo halitiliwi mkazo katika jamii nyingi hususani barani afrika huenda ni kutokana na malezi yasiyiridhisha au mwamko mdogo wa jamii kujitolea kwa ajili ya jamii zao.       Lakini hali imekuwa ni tofauti kwa waumini wa kanisa la waadventista wa sabato toka konferensi ya nyanda za juu kusini (SHC) wakiongozwa na mwenyekiti wa jimbo hilo  MCH. Kenan Mwasomola wamejitolea kujenga sehemu ya mabweni ya shule ya Mbeya adventist secondary school.

Mchungaji Kenan Mwansomola akiongoza waumini wa SHC katika kufyatua tofali za interlock.

     Waumini na washiriki hao toka mtaa wa mbalizi ili kufanikisha ujenzi huo wameanza zoezi la kufyatua matofari ya Interrock Kwa ajili ya Ujenzi wa Mabweni ya Mbeya Adventist Secondary School.
Ujenzi huu umekuwa ni katika  Kuitikia Wito wa Conference kwa washiriki wake Kujenga Shule  kwa kujitolea bila malipo Yoyote.

 

Sehemu ya matofali ambayo yatatumika katika ujenzi huo.( Picha zote kwa hisani ya idara ya mawasiliano SHC)

Washiriki hao wameahidi  kuwa Watatekeleza ujenzi huo wa Mbeya Adventist Secondary na kuezeka paa jipya bila malipo yeyote . Naye mwenyekiti wa SHC MCH. Kenan Mwasomola amesema sasa ni wakati wa washiriki kutumia Utaalam wetu kwa Kuwezesha Maendeleo ya Kanisa  hivyo kwa kushiriki ujenzi huu ameonesha mfano Kwa vitendo Umuhimu wa Kutumia nguvu kwa ajili ya Mungu kwa  kushiriki kufyatua Matofa ya Shule ya MASS.

Hivyo basi kwa namna waumini hawa walivyojitolea katika kufanikisha ujenzi huu jamii inapaswa iige mfano kwa kujitolea kwenye jamii za .Hongereni SHC kwa moyo mliouonesha.

No comments:

Post a Comment