KUTANA NA MWANAUME ALIYECHOMESHWA MAHINDI SIKU 10 AIRPORT



Wahenga walisema ama kweli mapenzi upofu hii imedhihirika wazi baada ya mwanaume mmoja  raia wa uholanzi kusafiri maili 5,400 ili kukutana na mpenzi wake  ambaye walikutana kwenye mitandao ya kijamii.
   Mwanaume huyo ajulikanaye kwa jina la Alexander Pieter Cirk, miaka 41 aliamua kusafiri umbali wote huo ili kukutana na mwanamke  raia wa china aitwaye Zhang na hatimaye kujikuwa akisubiri uwanja wa ndege kwa siku kumi pasipo kumwona mpenzi wake huyo.

 Lahaulaaaa baada ya kukaa kwa siku zote hizo pasipo kumuona ndio alipojikuta akikumbwa na uchovu mkubwa pamoja na mnyong'onyeo na kukaa kwa muda mrefu hali iliyopelekea apatiwe msaada wa matibabu ya haraka ili afya yake iweze kutengemaa



Kwa upande wake bibie Zhang akielezea kuhusu tukio hilo alisema kuwa hakudhani jambo hili linaweza kuwa ni hakika kwani imezoeleka kuwa jambo hilo laweza kuwa mzaha

(Picha zote kwa hisani ya mtandao)

 Bwana huyu ameonesha mapenzi ya kweli kwa mpenzi wake  je bado unaamini kuwa kuna mapenzi ya ukweli katika dunia hii? mtizamo wako ni upi katika hili tuambie ungekuwa wewe ungefanyaje?

No comments:

Post a Comment