Aliyekuwa mgombea wa urais nchini Marekani mwaka 2008 John McCain |
Wahenga walisema hujafa hujaumbika na usemi huo umedhihirika kwa mgombea wa urais wa chama cha
Republican 2008 ambaye kwa sasa ni seneta kupitia chama cha Republican bwana John McCain ambaye kwa sasa amegundulika kuwa na saratani ya ubongo.
Kwa mujibu wa ofisi yake imesemekana kuwa bwana McCain amegundulika kuwa na ugonjwa huo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa tishu ambao ulibaini kuwa seneta huyo ana uvimbe wa ubongo unaojulikana kama glioblastoma ulisababisha damu kuganda.
Ikumbukwe kuwa Glioblastoma ni uvimbe mbaya wa ubongo na mara nyingi huongezeka kutokana na umri wa mtu pia huathiri wanaume wengi zaidi ya wanawake.
Seneta huyo aliyehudumu kwa mihula sita ambaye pia alikuwa mwanajeshi aliyepigana vita nchini Vietnam ambaye pia aliwahi kutumikia miaka mitano jela yuko katika hali nzuri akiendelea kupata ahueni nyumbani kwake.
Hivyo basi ni wakati muafaka wa kumwomba Mungu ampatie afya njema bwana McCain ili aweze kupona mapema aweze kuwatumikia wananchi wake.
No comments:
Post a Comment