Tarehe 28 ya mwezi julai kila mwaka ni siku ya homa ya ini duniani ikumbukwwe kuwa ugonjwa huu umekuwa ni tatizo linalohitaji juhudi za pamoja ili kutokomeza ugonjwa huu.
ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya virusi ambavyo huingia mwilini kisha kushambulia ini na kupelekea kuwa maradhi sugu na endapo kama haujatibiwa hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha kansa ya ini na baadaye mgonjwa kupoteza maisha.
Ugonjwa huu hatari, na unaua idadi kubwa ya watu polepole kwani kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto kati ya watu 100, watu 8 wanaweza kuwa na maambukizi sugu na wasionyeshe dalili takwimu zilizopo zinaonyesha uwepo wa Maambukizi ya Virusi vya Hepatitis B na C nchini Tanzania.
Zipo njia kadhaa zinazochangia maambukizi ya ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na Kuchangia damu isiyo salama, Kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe mikasi, Kunyonyana ndimi nakadhalika
Kwa mujibu wa Waziri mwenye dhamana kati ya wachangiaji damu 200,000 waliochangia damu kwa mwaka 2016 asilimia 6 walikuwa na maambukizi ya Hepatitis B na asilimia 2 walikuwa na maambukizi ya Hepatitis C.
Hivyo basi ni jukumu la kila mtu kuhakikisha anapimwa na kupatiwa tiba mapema ili kukabiliana na ugonjwa huu
No comments:
Post a Comment