SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA KENYATTA


  1.        
    Rais mteule wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyata (picha kwa hisani ya mtandao)
    Novemba 28 mwaka 2017  itakuwa ni siku  ambayo taifa la Kenya haitasahau kwani  linatekeleza shughuli muhimu ya kikatiba ya kuapishwa kwa kiongozi wa taifa hilo kufuatia ushindi wake wa marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26 
  1. uliosusiwa na upinzani
  1.    Takriban viongozi wa mataifa yapatayo 13 wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo ambayo itafanyika mji mkuu wa nchi hiyo Nairobi  

  2. Rais Magufuli wa Tanzania, Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Edward Lowassa,Yoweri Museveni wa Uganda, Edgar Lungu wa Zambia, Mohamed Abdullah (Farmajo) wa Somalia na waziri mkuu wa Ethiopia Haile Mariam Desalegn ni miongoni mwa wageni waliofika Kasarani kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Bw Kenyatta.

         Wengine ni mama wa rais Uhuru Kenyatta Mama Ngina Kenyatta pamoja na wanachi wengine wa Kenya 


Raisi Kenyatta bado anakabiliwa na  Upinzani mkali nchini humo kwani mpinzani wake kutoka muungano wa NASA amewataka wafuasi wake kususia sherehe hiyo na badala yake kukusanyika katika mkutano ili kuwakumbuka wafuasi waliouawa katika ghasia tangu uchaguzi wa Agosti. 26


      Swali kubwa kwa wananchi wa kenya na afrika kwa ujumla je ataweza kuwaunganisha tena wakenya?

No comments:

Post a Comment