MAELFU YA RAIA WA DRC WAKIMBILIA ZAMBIA

     
bendera ya jamhuri ya kidemokrasia ya kongo ambayo zaidi ya wakazi wake 12000 wamekimbilia chini zambia (picha kwa hisani ya mtandao)

Zaidi ya watu 12 elfu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekimbilia nchini Zambia kutafuta hifadhi kutokana na machafuko  yanayoendelea Kusini Mashariki mwa nchi yao.

      Umoja wa Mataifa umesema  kuwa, hali ya wakimbizi hao ni mbaya, na wanakosa mahitaji muhimu kutokana na uhaba wa fedha 

Kuendelea kuongezeka kwa wakimbizi hao kunakuja  wakati ambapo chama kikuu cha upinzani nchini DRC, UDPS kinasema hakimtambui Waziri Mkuu Bruno Tshibala kama mwanachama na kiongozi ndani ya chama hicho.

Hatua hii inakuja baada ya Tshibala ambaye amewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho kusema kuwa anaandaa mkutano wa chama hicho kumteua kiongozi mpya wa UDPS baada ya kifo cha Ettien Tshisekedi mapema mwaka huu.

 Je unadhani ni nini hatima ya nchi hiyo katika duru za kimataifa?















No comments:

Post a Comment