Dk Salim Ahmed Salim aaga wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM


Salim Ahmed Salim ndio jina lake alizaliwa 23 Januari 1942 huyu ni mwanasiasa mkongwe kutoka Tanzania

Dr salim ni msomi mbobevu na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kuanzia tarehe 24 Aprili 1984 hadi tarehe 5 Novemba 1985. Akiwa  Waziri Mkuu wa tano wa Tanzania

Mbali na kutumika serikalini kwa kipindi kirefu Dkt. Salim Ahmed Salim ametumikia pia chama cha mapinduzi kwa muda mrefu hadi alipoamua kuwaaga  rasmi  Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye kikao kinachoendelea mjini Dodoma hapo jana.

Dkt. Salim ameaga baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitano ya kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho. 


Sambamba na kuaga huko Dr Salim  amempongeza Mwenyekiti wa CCM na rais wa jamhuri ya muumngano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa uongozi wake ambao umekiwezesha Chama kuimarika.

 Dkt. Salim pia amewashukuru wajumbe wote wa Kamati Kuu na viongozi wa Chama kwa ushirikiano ambao wamemwonesha muda wote wa ujumbe wake.

Aidha Mh. Dkt. Salim ameahidi kuendelea kushirikiana na kuwa mtiifu kwa Chama na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaongozwa na Chama cha Mapinduzi.


Dr Salim Ahmed Salim atakumbukwa kwa umahiri wake katika uongozi ndani na nje ya nchi uliopelekea kutunukiwa nishani mbalimbali ikiwemo Nishani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(1985)Nishani ya Kitaifa cha Vilima Elfu Moja (1993) na nyinginezo lukuki.

No comments:

Post a Comment