Kiongozi wa Buddha Dalai Lama |
Tenzin Gyatso ndio jina lake halisi lakini waumini wa dini ya buddha pamoja na watu wengine mbalimbali humwita Dalai Lama,
Alizaliwa eneo maarufu lililoko china lijulikanalo kama Tibet kiongozi huyu amekuwa akiishi uhamishoni kwa miongo sita sasa tangu Uchina ukandamize vuguvugu la Tibet.
Huyu ni miongoni mwa viongozi wa kidini wenye wafuasi wengi na ushawishi mkubwa kwa jamii huyu ndiye Dalai Lama kiongozi wa kidini wa Tibet mwenye umri wa miaka 82 anayeishi uhamishoni.
Dalai Lama amezindua programu tumishi ya simu kwa wafuasi wake ili iwawezeshe kufuatilia kwa karibu kuhusu mafunzo na safari zake.
Mbali ya program hii tumishi Dalai Lama ana akaunti ya Twitter iliyo na wafuasi zaidi ya milioni 16.
Application hiyo itaitwa, Dalai Lama na itapatikana bure kwa sasa pia inapatikana kwenye simu za iPhone pekee, na ataitumia kutoa mafundisho, video, picha na taarifa nyinginezo na inasemekana kuwa hadi sasa App hiyo haijakaguliwa sana na watumiaji.
Mara zote Dalai Lama amekuwa akihubiri amani na uvumilivu wa kiimani kwa waumini wa Buddha na anashinikiza kujitawala kwa Tibet iliyomo ndani ya China lakini utawala wa China unamuona kuwa mtu anayeshinikiza kugawanayika kwa nchi hiyo
Mwaka 1989 alishinda tuzo ya Nobel ya amani
No comments:
Post a Comment