![]() |
Mheshimiwa Joel Bendera (Picha kwa hisani ya mtandao) |
Akithibisha kutokea kwa kifo hicho msemaji wa hospitali ya taifa Muhimbili Aminiel Aligaesha ambaye ni msemaji wa hospitali hiyo amesema, “Ni kweli Joel Bendera amefariki aliletwa leo (jumatano) na gari la wagonjwa saa 6:30 mchana na ilipofika saa 10:24 jioni alifariki.”
Mh Bendera mbali ya ukuu wa mkoa, amewahi pia kuwa mbunge wa Korogwe Mjini na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo katika utawala uliopita wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.
Mh Bendera alikuwa miongoni mwa wastaafu katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa yaliyofanywa na Rais John Magufuli Oktoba 26,2017 na nafasi yake kuchukuliwa na Mh Alexander Mnyeti aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
Mkoani Manyara Mheshimiwa Bendera atakumbukwa kwa moyo wake wa kuhamasisha mazoezi ya viungo na michezo kwa ujumla pia atakumbukwa na wanamichezo wote na wapenzi wa kandada kama kocha bora wa timu ya taifa (TAIFA STARS).
Pumzika vyema Mh Joel Bendera
No comments:
Post a Comment