Waziri wa ofisi ya Rais TAMISEMI Mh Selemani Jafo |
Wanafunzi takribani 650,862 kati ya wote waliofanya mtihani mwaka huu ndio waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza
Akiongea na waandishi wa habari waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo, amesema kuwa jumla ya wanafunzi 650,862 ambao ni sawa na asilimia 98.31 ndio wamefanikiwa kuchaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza mwaka 2018.
Waziri Jafo amesema kuwa wanafunzi wengine 11,173 ambao ni sawa na asilimia 1.69 ya waliofaulu hawakuweza kupata nafasi ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika awamu hiyo kutokana na uhaba wa miundombinu ikiwemo vyumba vya madarasa.
Aidha waziri Jafo amesema kuwa mwaka huu idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza imeongezeka kwa 124,209 likiwa ongezeko la asilimia 23.58.
Aidha, amesema baadhi ya wanafunzi wa mikoa ya Lindi, Mbeya, Rukwa, Manyara, Katavi na Simiyu, wamekosa nafasi kutokana na uhaba wa miundombinu ya elimu katika mikoa yao vikiwemo vyumba vya madarasa.
No comments:
Post a Comment