KWA HALI HII YA JOTO 2016 NINI KIFANYIKE?

  Huenda unaweza kujiuliza ni nini hasa ikawa ni chanzo cha haya yote na nini kinachosababisha hali hii lakini ukakosa jibu linaloridhisha kuhusu hali ya joto inayoendelea kuongezeka duniani
Kiwango cha joto kwa mwaka huu wa 2016 huenda kikaongezeka na kuwa na hali ya  joto zaidi ulimweguni ukilinganisha na takwimu za mwaka jana na  hapo awali.
 Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na  masuala ya Hali ya Hewa mwaka huu utavunja rekodi kwa kuwa na kiwango cha juu cha joto, tangu kuanza kwa vipimo vya hali ya hewa katika karne ya 19. 
       Kihistoria Mwaka wa 1998 ndio mwaka pekee ambao haukushuhudia kiwango kikubwa cha joto ulimwenguni.
         Shirika hilo limesema  kuwa takwimu za mwezi Oktoba zinaonesha kuwa wastani wa joto duniani kwa mwaka huu ni nyuzi joto 1.2 za Celsius. 
      Kiwango hicho kinafikia kile kilichowekwa katika makubaliano ya hali ya hewa duniani yaliyofikiwa mjini Paris, Ufaransa mwaka uliopita. 
     Imeelezwa kuwa kiwango hiki cha joto kimesababishwa na  El Nino na kuvunja rekodi ya mwaka 2015 ambao ndio  ulikuwa mwaka wenye joto kali zaidi. 
   Mbali ya  El Nino sababu nyingine ni utoaji wa gesi chafu ya kaboni ambayo inaharibu tabaka la ozone ambalo hutumika kuzuia mionzi ya jua .
 Je unadhani hadi kufikia hapa ni wapi tulipokosea na je nini kifanyike kukabiliana na hali hii?




No comments:

Post a Comment