Jafoo aajiri walimu wapya 3,033

   
Ualimu umekuwa ni taaluma muhimu katika maisha waalimu wathaminiwe (Picha na Mwananchi)
Ikiwa ni miezi kadhaa tangu kuwepo kwa zoezi la uhakiki wa watumishi wa serikali, zoezi hilo limezaa matunda na kupelekewa kuondolewa kwa watumishi ambao hawakuwa na sifa  na kubainisha pia wale ambao ni watumishi hewa.

  
Sekta ya elimu pia imekuwa ni miongoni mwa sekta ambazo zimeathiriwa na zoezi hili na kupelekea kuwepo na upungufu wa walimu.

      Kufuatia upungufu huo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ametangaza ajira mpya 3,033 za walimu wa shule mbalimbali nchini za msingi na Sekondari ambao watakwenda kujaza nafasi za walimu waliobainika kuwa na vyeti feki.

     Mh Jafo ametangaza  majina ya walimu hao wapya 3,033 hapo jana  na kuwapangia vituo vya kazi walimu 266 wakiwa ni walimu wa shule za sekondari na Walimu 2,767 watakuwa walimu wa shule za msingi.

      Aidha Jafo amewataka walimu hao wapya ambao wamechaguliwa kuripoti kwa Wakurugenzi wa halmshauri husika ambazo watakuwa wamepangiwa kuanzia Disemba 27, 2018 hadi Januari 7, 2018.


     Mh Jafo pia amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo walimu hao wataripoti hapo baadaye  kuwapokea na kuzingatia taratibu na kanuni zote za utumishi wa Umma na baadaye kutoa taarifa ya kuripoti kwao.

No comments:

Post a Comment