- Askofu mkuu wa kanisa la waadventista wa sabato duniani mchungaji Ted Wilson amewaomba waumini na washiriki wa kanisa hilo dunia nzima kuweza kuwaombea washiriki wenzao walioko katika nchi za afghanistan,armenia,Tajikistan na nyinginezo zinazounda divisheni ya ulaya na asia ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kazi ya utume.
- Hayo ameyasema kupitia chapisho lake katika mtandao wa twitter ikiwa ni katika kuelekea mkutano wa mwaka ambapo utaenda sambamba na mfululizo wa maombi kwa ajili ya kuombea kazi ya utume inayoendelea duniani kote.
Amesema shauku kubwa ya washiriki na waumini wa divisheni hii ni kuweza kupata mbinu mpya za uinjilisti baada ya serikali za baadhi ya nchi zinazounda divisheni hii kuzuia mikutano ya hadhara, pia waweze kupata mahali bora pa kuabudu kwani kwa sasa washiriki na waumini husali katika majengo ya kukodi. Amesisitiza kuwa dunia inapokuwa ikikaribia ukingoni ni wajibu wa kila mshiriki na muumini kuweza kushiriki katika kazi ya utume kama lilivyo agizo la injili.
Je unashiriki kwa namna gani kwa ajili ya ndugu na jamaa ambao bado hawajaujua ukweli?
No comments:
Post a Comment