JE WAJUA HALI YA ULEVI KWA VIJANA ILIVYO NCHINI JAPAN ?


       

(Bendera ya nchi ya japan ambapo hali ya ulevi miongoni mwa vijana imepungua kwa kiasi kikubwa. picha kwa hisani ya mtandao.)

     Suala la ulevi miongoni mwa vijana  nchini Tanzania limekuwa ni suala linalokua siku hadi siku hivyo kupelekea kuwa janga la kitaifa siku za mbeleni endapo halitapatiwa ufumbuzi mapema,     Pombe mbali ya kuharibu mustakabali wa maisha ya vijana wengi lakini pia imechangia katika vitendo vingi vya uhalifu ikiwemo
  •  wizi, 
  • ukabaji na
  •  hata vitendo vya ubakaji ambavyo vinachangia maambukizi ya virusi vya ukimwi
      Lakini huko nchini Japan hali ni tofauti kwani  Wizara ya Afya, Ajira na Ustawi wa Jamii ya Japan imefanya utafiti na kubaini kuwa tabia ya vijana wengi wa japani wanaokunywa pombe mara kwa mara, imepungua kwa zaidi ya nusu katika kipindi cha miaka kumi iliopita  Katika Utafiti huo uliolenga katika idadi ya watu wanaokunywa pombe kwa takribani mililita 500 za bia au mililita 60 za pombe kali angalau kwa siku tatu kwa wiki. ulibaini kuwa sababu kubwa iliyosaidia kupunguza ulevi ni kwamba watu wengi nchini  Japan 
  • wamekuwa wakitilia maanani afya zao. 
  • Ulevi kwa wanaume, uwiano wa wanywaji wa kila siku umeshuka si tu miongoni mwa wale waliopo kwenye miaka ya 20 lakini pia miaka ya 30, 40 na 50
  • wafanyakazi  wengi vijana wanaaminika kuwa hawapendi unywaji wa pombe 
  • . Kutokana na kuongezeka kwa ugumu wa kupata ajira baada ya kuhitimu masomo, waajiriwa wapya wanaonekana kutafuta maelewano mazuri na waajiri wao.

Hivyo basi sasa ni wakati wa kila mtanzania na serikali kwa ujumla kuweza kujifunza kitu kwa nchi ya japani kwani kama suala la ulevi kwa vijana lisipovaliwa njuga tutajikuta tunakuwa na kizazi kilichojaa vijana waraibu wa pombe. Je wewe kama mwanajamii unadhani serikali ifanye nini kukabiliana na suala hili?

No comments:

Post a Comment