Ikiwa ni siku chache tangu kuingia sokoni kwa simu za iPhone 7 na iPhone 7 plus na kujipatia umaarufu mkubwa duniani hali imekuwa tofauti huko nchini China kwani kampuni kadha nchini humo zimetoa onyo kali kwa wafanyakazi wake na kuwataka wasinunue simu hizo.
Msemaji wa kampuni ya Nanyang Yongkang Medicine ambayo ni miongoni mwa kampuni iliyozuia wafanyakazi wake kununua simu hii Bw Liu amesema, lengo la agizo hilo ni kuwahamasisha wafanyakazi kujali zaidi familia zao badala ya kuhangaikia vitu vya anasa.
Mbali ya kampuni hiyo hospitali ya Fuling Xinjiuzhou Gynecology Hospital ya mjini Chongqing imewaonya wafanyakazi wake wasinunue iPhone7. kwani bei yake ni ya juu mno ukilinganisha na simu nyingine.
Pia ili kuendeleza utamaduni kwa kutopenda matumizi ya anasa na kutumia pesa kwa busara, wasimamizi wa hospitali wamefikia uamuzi wa kuwapiga marufuku wafanyakazi wetu wasinunue simu za iPhone7.
Kwa upande mwingine baadhi ya watu wamekuwa na mtizamo tofauti na kutoa mtizamo wao kupitia mtandao wa Weibo wameeleza kwamba kususia iPhone7 huenda kukawa kunawadhuru Wachina wenyewe kwani uzalishaji wa simu za Apple hufanywa katika viwanda vya kampuni ya Foxconn nchini China.
Baadhi ya watu wanaotetea uzalendo wa Wachina wamekuwa pia wakipinga simu za iPhone kuonyesha kutoridhishwa kwao na uamuzi wa jopo la kimataifa uliosema China haina haki ya kumiliki visiwa ambavyo imekuwa ikidai katika bahari ya South China Sea hivyo kusababisha baadhi yao kuharibu simu zao hadharani kama sehemu ya kupinga hilo
Baadhi ya watu wanaounga mkono uzalendo wa nchi ya china wakiharibu simu zao hadharani kama sehemu ya kuunga mko uzalendo. (Picha kwa hisani ya mtandao wa WEIBO) Huo ndio uzalendo wa wananchi wa china kuhusu bidhaa za Apple hususani simu mpya za iPhone 7 na iPhone 7 plus je unadhani wanachofanya kitaathiri vipi biashara na uchumi kwa ujumla |
No comments:
Post a Comment