Yaliyomuudhi Mwigulu mwaka 2017 ni haya


Mbunge wa Iramba magharibi na waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mheshimiwa  Mwigulu Nchemba amesema kwamba miongoni mwa matukio  yaliyomuudhi sana mwaka 2017 ni pamoja na tukio la kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo Mh Tundu Lissu.

Mbali ya tukio la kushambuliwa kwa Lissu  mauaji ya wananchi na Askari huko Kibiti pia ni jambo jingine ambalo lilitikisa vichwa vya habari nchini Tanzania.

Mh. Mwigulu Nchemba ambaye ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi  ameyasema hayo wakati  akiongea na waandishi wa habari mkoani Dodoma.


Waziri huyo pia ametoa mwelekeo wa wizara ya mambo ya ndani ya  nchi kwa mwaka mpya wa 2018 nini kama wizara wamejipanga kufanya.

Aliyoyasema JPM baada ya Babu Seya kumtembelea ikulu


Mwanamuziki maarufu Nguza Viking almaarufu kama Babu Seya aikiongozana na wanawe leo hii wamemtembelea Rais wa jamhuri ya muungano Dkt John Magufuli ikulu kwa lengo la kumshukuru baada yake kuwaachilia huru kwa msamaha wa rais desemba 9 mwaka huu.

Hapo awali Nguza Viking pamoja na mwanae walikuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela hadi walipotoka kwa msamaha wa raisi desemba 9 mwaka huu

Hivyo basi kama sehemu ya shukrani leo hii wameamua kumtembelea Dkt Magufuli ili waweze kutoa shukrani zao ambapo mbali na mazungumzo mengine Dkt magufuli amewaambia kuwa shukrani za pekee zimwendee Mwenyezi Mungu kwani yeye ndiye husamehe.



Kichanga chaokotwa mkesha wa mwaka mpya 2018


Kila mtoto anayezaliwa anatamani aishi hivyo jamii inapaswa kuwalinda watoto.( Picha na mtandao)
Mwaka unapoanza kila mtu hujawa na fura na kumshukuru Mungu kwa kuweza kuuona mwaka mwingine.
Wengi wetu hufurahia afya njema pamoja na uhai tunaokuwa nao lakini hali imekuwa tofauti katika mkesha wa mwaka 2018 kwani  mtoto mchanga wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa siku tatu ameokotwa akiwa amekufa baada ya kutupwa  kwenye kichaka eneo la Tandale na watu wasiojulikana.
 Kwa mujibu wa Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Mwananyamala Bi. Jasmine mwili wa  mtoto huyo umeokotwa na jeshi la polisi na kwa sasa  uhifadhiwa katika hospitali hiyo.
Muuguzi huyo amesema mbali ya tukio hilo la kinyama  jumla ya watoto saba wamezaliwa usiku wa kuamkia mkesha wa mwaka mpya wa 2018.

Jafoo aajiri walimu wapya 3,033

   
Ualimu umekuwa ni taaluma muhimu katika maisha waalimu wathaminiwe (Picha na Mwananchi)
Ikiwa ni miezi kadhaa tangu kuwepo kwa zoezi la uhakiki wa watumishi wa serikali, zoezi hilo limezaa matunda na kupelekewa kuondolewa kwa watumishi ambao hawakuwa na sifa  na kubainisha pia wale ambao ni watumishi hewa.

  
Sekta ya elimu pia imekuwa ni miongoni mwa sekta ambazo zimeathiriwa na zoezi hili na kupelekea kuwepo na upungufu wa walimu.

      Kufuatia upungufu huo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ametangaza ajira mpya 3,033 za walimu wa shule mbalimbali nchini za msingi na Sekondari ambao watakwenda kujaza nafasi za walimu waliobainika kuwa na vyeti feki.

     Mh Jafo ametangaza  majina ya walimu hao wapya 3,033 hapo jana  na kuwapangia vituo vya kazi walimu 266 wakiwa ni walimu wa shule za sekondari na Walimu 2,767 watakuwa walimu wa shule za msingi.

      Aidha Jafo amewataka walimu hao wapya ambao wamechaguliwa kuripoti kwa Wakurugenzi wa halmshauri husika ambazo watakuwa wamepangiwa kuanzia Disemba 27, 2018 hadi Januari 7, 2018.


     Mh Jafo pia amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo walimu hao wataripoti hapo baadaye  kuwapokea na kuzingatia taratibu na kanuni zote za utumishi wa Umma na baadaye kutoa taarifa ya kuripoti kwao.

Mikoa minne ya Tanzania kukumbwa na mvua kubwa

     
Mara nyingi panapokuwepo na mvua kubwa huleta athari kwa watu na mali (Picha na mtandao)
Zikiwa zimebaki siku chache kuumaliza mwaka 2017 mamlaka  ya Hali ya Hewa Tanzania imesema kuelekea  mwisho wa mwaka huu  mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha katika mikoa minne ya Tanzania  ambayo ni  Rukwa Mbeya, Songwe na Kigoma.
   Hayo yamesemwa na Meneja wa Kituo Kikuu cha Utabiri wa Hali ya Hewa  Bwana Samuel Mbuya na kueleza kuwa  mikoa hiyo minne ndio inatarajiwa kuwa na mvua wakati huu wa mwisho wa mwaka  na kwa mikoa mingine ya Pwani na Dar es salaam ifikapo mwisho wa mwezi huu, mvua za vuli zinazoendelea kunyesha mikoa hiyo  zitakuwa zimefikia ukingoni.
      Meneja huyo amesema kuwa mamlaka ya hali ya hewa inatarajia mvua zitaendelea kunyesha katika maeneo ya mikoa ya Magharibi ambayo ni Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Ruvuma, Lindi, Dodoma na Singida ambazo  zilianza kunyesha Novemba  zinatarajiwa kumalizika Aprili.
        Mbuya amesema maeneo mengine katika mikoa ya Tanzania  kutakuwa na mvua za kawaida huku mikoa minne ikiwa na mvua kubwa.
         Aidha bwana Mbuya  amewataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa  mara kwa mara ili wapate  mwelekeo wa hali ya hewa na tahadhari wanazotakiwa kuchukua.

Bodi ya udhamini ya EAGT yawasimamisha kazi viongozi wakuu wa kanisa hilo.



      Bodi ya Wadhamini ya Kanisa la Evangelistic Assemblies Of God Tanzania (EAGT)  imemsimamisha Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Mchungaji Brown Mwakipesile ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
       Wengine waliosimamishwa leo Desemba 18 ni Katibu Mkuu, Mchungaji Leonard Mwizarubi na Mhasibu Mkuu, Mchungaji PrayGod Mngonja.
       Pamoja na mabadiliko hayo, bodi imewateua kwa muda kushika nafasi hizo, Askofu Mkuu atakuwa ni Mchungaji Asumwisye Mwaisabila, Katibu Mkuu atakuwa Dk Jakob Madaha na Mhasibu Mkuu atakuwa Andrea Salu.
        Kwa mujibu wa Katiba ya EAGT ya Mwaka 2011 ,ibara ya 6(b)(5) kinatoa mamlaka Kwa Wajumbe wanne wa bodi hiyo kusimamisha viongozi wakuu wa kanisa akiwamo Askofu Mkuu kabla ya Mkutano Mkuu kujadili maazimio hayo.
       "Baada ya siku 30 tutakuwa na mkutano mkuu wa Kanisa kwa ajili ya kupitisha mabadiliko hayo, wamesimamishwa kwa kumfukuza Makamu Askofu Mkuu wakidai alitenda dhambi, walimfukuza uchungaji na uumini pia," ni kauli ya Mwenyekiti wa bodi hiyo, John Mfuko alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
        Mzee Mfuko ambaye anazungumza kwa taabu kutokana na umri wake alisema  kosa la viongozi hao wa kanisa ni kumfukuza bila kushirikisha bodi ya Wadhamini.
        Mzee Mfuko aliyeongozana na wajumbe wawili kati ya wanne wa bodi hiyo alisema  licha ya mahakama kubatilisha suala la kumfukuza, Askofu Mkuu (aliyefukuzwa)  alikataa kumrejesha kanisani. Tuhuma nyingine ni kushiriki njama za kuhujumu mali za kanisa.
        Mbali na tuhuma hizo, bodi imewataka waumini wa kanisa hilo kutotuma pesa katika akaunti za kanisa huku ikiweka wazi kushikilia akaunti hizo kutoka mikononi mwa viongozi waliokuwa na dhamana ili kuhakiki wa mali za kanisa.

Kongamano la kimataifa la Kiswahili lazinduliwa Zanzibar

     

Lugha ya kiswahili imekuwa 
lugha rasmi ya serikali na taifa la Tanzania  hutumika katika shule za msingi  lakini shule za upili na vyuoni hutumika katika shughuli za kawaida na ligha ya   Kiingereza hutumika kufundishia. 
     Mnamo tarehe 15 Februari 2015 rais mstaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete alitangaza mpango wa kubadilisha lugha ya elimu nchini kwa kutumia Kiswahili kwenye ngazi zote hadi shule za sekondari na chuo kikuu hii ikiwa ni katika kukuza na kuenzi lunga ya kiswahili
      Leo hii rais wa serikali ya mapinduzi ya  Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, anazindua kongamano la kimataifa la Kiswahili linalofanyika katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi la zamani mjini Unguja.
    Taarifa iliyotolewa  na Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (Bakiza), Mohamed Seif Khatib imesema kuwa kongamano hilo la siku mbili litajadili mada 100 zitakazowasilishwa na wageni, zikiwamo makala maalumu zinazohusiana na lugha ya kiswahili
       Mwenyekiti huyo amebainisha tamasha hilo linatazamiwa kuwa na  washiriki wapatao 100 wakiwamo wataalamu wa Kiswahili wa ndani na nje ya nchi, taasisi za kiraia, wataalam na wanafunzi kutoka vyuo vikuu pamoja na wananchi.
       Kwa upande wake katibu mtendaji wa baraza hilo, Mwanahija Ali Juma aliwataka wananchi kuchangamkia fursa ya kongamano hilo kwa kushiriki ili nao waweze kuongeza utaalamu zaidi katika kutumia misamiati ya lugha yao.

Dk Salim Ahmed Salim aaga wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM


Salim Ahmed Salim ndio jina lake alizaliwa 23 Januari 1942 huyu ni mwanasiasa mkongwe kutoka Tanzania

Dr salim ni msomi mbobevu na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kuanzia tarehe 24 Aprili 1984 hadi tarehe 5 Novemba 1985. Akiwa  Waziri Mkuu wa tano wa Tanzania

Mbali na kutumika serikalini kwa kipindi kirefu Dkt. Salim Ahmed Salim ametumikia pia chama cha mapinduzi kwa muda mrefu hadi alipoamua kuwaaga  rasmi  Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye kikao kinachoendelea mjini Dodoma hapo jana.

Dkt. Salim ameaga baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitano ya kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho. 


Sambamba na kuaga huko Dr Salim  amempongeza Mwenyekiti wa CCM na rais wa jamhuri ya muumngano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa uongozi wake ambao umekiwezesha Chama kuimarika.

 Dkt. Salim pia amewashukuru wajumbe wote wa Kamati Kuu na viongozi wa Chama kwa ushirikiano ambao wamemwonesha muda wote wa ujumbe wake.

Aidha Mh. Dkt. Salim ameahidi kuendelea kushirikiana na kuwa mtiifu kwa Chama na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaongozwa na Chama cha Mapinduzi.


Dr Salim Ahmed Salim atakumbukwa kwa umahiri wake katika uongozi ndani na nje ya nchi uliopelekea kutunukiwa nishani mbalimbali ikiwemo Nishani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(1985)Nishani ya Kitaifa cha Vilima Elfu Moja (1993) na nyinginezo lukuki.

Application ya Dalai Lama yazinduliwa rasmi

Kiongozi wa Buddha Dalai Lama
Tenzin Gyatso  ndio jina lake halisi lakini waumini wa dini ya buddha pamoja na watu wengine mbalimbali humwita Dalai Lama, 
Alizaliwa eneo maarufu lililoko china lijulikanalo kama Tibet kiongozi huyu amekuwa akiishi uhamishoni kwa miongo sita sasa tangu Uchina ukandamize vuguvugu la Tibet.
Huyu ni miongoni mwa viongozi wa kidini wenye wafuasi wengi na ushawishi mkubwa kwa jamii huyu ndiye Dalai Lama kiongozi  wa kidini wa Tibet mwenye umri wa miaka 82 anayeishi uhamishoni. 
Dalai Lama amezindua programu tumishi ya simu kwa wafuasi wake ili iwawezeshe kufuatilia kwa karibu kuhusu mafunzo na safari  zake.
Mbali ya program hii tumishi Dalai Lama ana akaunti ya Twitter iliyo na wafuasi zaidi ya milioni 16.
Application hiyo itaitwa, Dalai Lama na itapatikana  bure kwa sasa pia inapatikana kwenye simu za iPhone pekee, na ataitumia kutoa mafundisho, video, picha na taarifa nyinginezo na inasemekana kuwa hadi sasa  App hiyo haijakaguliwa sana na watumiaji.
    Mara zote Dalai Lama amekuwa akihubiri amani na uvumilivu wa kiimani kwa waumini wa Buddha na  anashinikiza kujitawala kwa Tibet iliyomo ndani ya China lakini utawala wa China unamuona kuwa mtu anayeshinikiza kugawanayika kwa nchi hiyo


    Mwaka 1989 alishinda tuzo ya Nobel ya amani